WASHINGTON DC, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameionya Oman akisema hatosita kutuma jeshi lake kuishambulia kwa mabomu endapo itaendelea kujihisha na mgogoro wa Iran.
Wakati huo huo, Rais Trump amedai kuwa yapo mazungumzo mazuri yanayoendelea kati ya Marekani na jeshi la Mapinduzi ya Kiislam la Iran (IRGC).
Kwa upande wake, Oman imekuwa ikiweka wazi kuwa haina upande, ingawa imeshambuliwa mara kadhaa na Iran.
Licha ya kushambuliwa huko, Oman imekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza amani kati ya Marekani na Taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, kile kinachotajwa kuwa ndiyo sababu ya Rais Trump kuipa onyo, Oman inatajwa kukaa mezani na Iran ili kuishawishi kuufungua Mlango-Bahari wa Hormuz.


