Na mwandishi wetu, Gazetini
SEKTA hii itachukua nafasi muhimu katika kuendesha maendeleo ya Tanzania, hususan katika maeneo ya biashara, huduma za ukarimu, na huduma zingine za kijamii na kiuchumi.
Kuongezeka kwa watu wenye kipato cha kati kutaongeza mahitaji ya biashara na huduma, hivyo kuchochea ajira, kupanua fursa za biashara, na kuimarisha shughuli za kiuchumi.
Ili kutumia fursa hizi kikamilifu, Tanzania italazimika kuwekeza katika mafunzo, miundombinu na majukwaa ya kidijitali.
Wakati huo huo, ni muhimu kuweka kanuni za kuwalinda watumiaji na kuhakikisha kwamba kunakuwa na ushindani kwa manufaa kwa watumiaji.
Ni kwa maana hiyo, sekta hii ya huduma ina umuhimu mkubwa katika kuyafikia maendeo ya uchumi nchini ifikapo mwaka 2050.


