LONDON, Uingereza
BAADA ya kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu uliopita (2025-26), Mohamed Salah amesaini mkataba wa miaka miwili na Trabzonspor ya Ligi Kuu ya Uturuki.
Uamuzi wake wa kwenda Uturuki, licha ya kutakiwa na klabu kubwa za Ulaya, ikiwamo PSG, umekumbana na ukosolewaji mkubwa, wengine wakisema ‘amepotea’.
Miongoni mwa waliokuwa wamepinga usajili huo ni beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, aliyedai kuwa soka la Uturuki liko chini kuliko uwezo wa Salah.
Hata hivyo, straika wa zamani wa Arsenal na Manchester City, Emmanuel Adebayor, ameibuka na mtazamo tofauti, akisema Salah amefanya uamuzi sahihi.
“Ni jambo zuri kumuona Mo Salah akiwa Uturuki. Anakwenda kuendeleza historia ya soka la Afrika katika nchi hii,” amesema Adebayor.
Kwa upande wake, Adebayor raia wa Togo amewahi pia kukipiga Ligi Kuu ya Uturuki akiwa na Istanbul Basaksehir (2017-18) na Kayserispor (2019).


