23 C
New York

Sekta za Mageuzi zinazoibeba Dira 2050: Michezo na Ubunifu

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SEKTA hizo zina uwezo mkubwa ambao haujatumiwa kikamilifu katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Sekta hizi zinatoa fursa muhimu kwa ajira za vijana wengi nchini.

Pia, mbali ya kuzalisha ajira na kuendeleza ujuzi, sekta hizi zina mchango mkubwa katika kujenga umoja na mshikamano katika jamii.

Tanzania inalenga kuwa kitovu cha utamaduni, sanaa bunifu na michezo barani Afrika ifikapo mwaka 2050, ikiwa na sekta zinazostawi katika muziki, filamu, mitindo, na burudani.

Kwa kukuza vipaji na kuweka mazingira wezeshi, Tanzania itafungua milango ya ubunifu na ujasiriamali kwa vijana.

Sambamba na hayo, uwekezaji kwenye mifumo ya haki za uvumbuzi utakuwa muhimu ili kuhakikisha kwamba sekta hizi zinashamiri na kuwa endelevu.

Related articles

Recent articles