9.5 C
New York

Utafiti waonesha mafuta yanaweza kupatikana ndani ya Tanzania Bara

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini, Arusha

UTAFITI unaofanyika katika mradi wa kimkakati wa Eyasi Wembere, unaolenga kutafuta mafuta na gesi katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, umeonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa rasilimali hizo katika eneo hilo.

Hayo yamebainika wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo wilayani Karatu, mkoani Arusha.

“Kazi za utafiti wa mradi huu zilianza mwaka 2015. Tumekuwa tukikusanya data mbalimbali zinazohusiana na uwepo wa mafuta na gesi, ambapo baada ya uchambuzi tulibaini kuwa katika eneo hili la bonde ipo miamba tabaka yenye uwezo wa kuhifadhi mafuta,” amesema Dk. Mataragio.

“Kazi za utafiti wa mradi huu zilianza mwaka 2015. Tumekuwa tukikusanya data mbalimbali zinazohusiana na uwepo wa mafuta na gesi, ambapo baada ya uchambuzi tulibaini kuwa katika eneo hili la bonde ipo miamba tabaka yenye uwezo wa kuhifadhi mafuta,” amesema Dk. Mataragio.

Ameeleza kuwa utafiti wa awali uliofanyika mwaka 2015 kwa kutumia ndege na visima vifupi uligharimu takribani shilingi bilioni nane, huku awamu ya kwanza ya utafiti kwa njia ya mitetemo yenye urefu wa kilomita 260 ikigharimu sh bilioni 10.

Ameongeza kuwa awamu ya pili ya utafiti itahusisha eneo lenye urefu wa kilomita 914 na kugharimu shilingi bilioni 43, ambapo hadi sasa kilomita 430 zimekamilika, sawa na asilimia 47 ya kazi yote.

Akizungumzia manufaa yatakayopatikana endapo mafuta yatagunduliwa, Dkt. Mataragio alisema hatua hiyo itapunguza gharama za ununuzi wa mafuta nje ya nchi na kusaidia kutunza akiba ya fedha za kigeni.

“Tutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta nchini na pia tutaokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta nje ya nchi,” ameongeza Dk. Mataragio.

Amesema tangu kuanza kwa mradi huo mwaka 2015, zaidi ya asilimia 90 ya wanaotekeleza kazi ni Watanzania.

Baada ya ukaguzi wa mradi, Dk. Mataragio aliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na mkandarasi kampuni ya African Geophysical Services (AGS) kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kabla ya mwezi Aprili 2026, na kwamba kazi ziendelee hata kipindi cha mvua.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utafutaji, Uendelezaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, Mjiolojia Paschal Njiko, alisema shirika hilo linafanya utafiti huo kwa ushirikiano na AGS, na litaendelea kumsimamia mkandarasi kuhakikisha awamu ya pili inakamilika kwa wakati.

Naye, Mwenyekiti wa AGS, Salum Haji, alisema wanatambua umuhimu wa mradi huo kwa taifa na watahakikisha kazi inakamilika kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake, mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Biru Benjamini, alisema:“Kupitia mradi huu, sisi vijana tuliokuwa mitaani tumenufaika kwa kupata ajira na ujuzi.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img