12.5 C
New York

Dk. Samia: Tokeni kifua mbele, hakuna wa kuwatisha Oktoba 29

Published:

Na Mwandishi Maalum, Gazetini

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa hakuna kitakachotokea Oktoba 29, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kifua mbele kwenda kupiga kura.

Hii ni zaidi ya mara ya tatu kwa Dk. Samia kutoa hakikisho hilo kwa Watanzania, akibainisha kuwa vyombo vya dola na Serikali vimejipanga vizuri kudhibiti jaribio lolote litakalolenga kuathiri upigaji kura.

Dk. Samia ameyasema hayo, Jumamosi Oktoba 11, 2025, alipohutubia mkutano wa kampeni za urais uliofanyika wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

“Nimeona Kahama wapigakura ni wengi mno, na wale jamaa zetu wanaweza kujaribu kutoa vitisho ili kura zisiwe nyingi. Nataka kuwaambia, tokeni kifua mbele tarehe 29, hakuna litakalotokea. Mnaowaona pale, walinzi wetu wamejipanga vizuri mno.

Kila kitu kiko salama—tokeni mkapige kura,” amesema Dk. Samia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano huo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img