14.7 C
New York

‘Putin hataki amani Ukraine’

Published:

KYIV, Ukraine
KATIBU Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi (NATO), Anders Fogh Rasmussen, haoni kama Urusi ina nia ya kurejesha amani nchini Ukraine.
Kwa miezi kadhaa sasa, Urusi na Ukraine zimekuwa kwenye vita inayogharimu maisha ya raia wengi wasio na hatia, achilia mbali uharibifu wa miundombinu ya usafiri na majengo.
Hivi karibuni, Rais wa Marekani, Donald Trump, alikutana na mwenzake wa Urusi, Vladmir Putin, ajenda ikiwa ni namna ya kumaliza mgogoro huo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Fogh Rasmussen ambaye kwa sasa ni mshauri wa Serikali ya Ukraine, Rais Putin hataki kuona amani ikirejea.
“Urusi inapata masilahi kupitia uwanja wa vita, hivyo haina mpango wa kuacha. Unadhani Urusi inaweza kuacha vita kwa sasa? Hapana.
“Hata kama Ukraine itapewa silaha zote, pamoja na misaada ya kifedha ili kuirudisha nyuma Urusi. Ikiwa bado Putin anaamini atashinda, basi vita itaendelea,” alisema Fogh Rasmussen.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img