KABUL, Afghanistan
WAHAMIAJI 37, wakiwamo watoto 17, waliokuwa wakirejeshwa kutoka Iran wamefariki baada ya gari lao kupata ajali Magharibi mwa Afghanistan.
Ofisi Habari wa Taliban, Ahmadullah Mottaqi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema ilitokana na basi la wahamiaji hao kuwaka moto baada ya kugongana na lori la mizigo na pikipiki.
Kwa miezi ya hivi karibuni, Iran imekuwa ikiwarudisha wahamiaji walioingia nchini humo wakikimbia machafuko Afghanistan.
“Abiria wote waliokuwamo kwenye basi ni wahamiaji waliochukua usafiri huo mjini Islam Qala,” alisema Gavana Mohammad Yousuf Saeedi akihojiwa na AFP.
Kwa upande mwingine, taarifa ya polisi imeeeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe na mwendo kasi wa dereva, kwa mujibu wa Shirika hilo la Habari.
Hata hivyo, ajali za barabarani si jambo geni Afghanistan, ikichangiwa zaidi na uharibifu wa miundombinu unaotokana na vita.
Published:


