18 C
New York

Stars ni rekodi za kibabe tu CHAN 2024

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
KWA mara ya kwanza katika historia ya CHAN, timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetinga robo fainali, tena ikimaliza hatua ya makundi ikiwa kileleni mwa msimamo.
Licha ya suluhu dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jana, bado Stars ilimaliza kileleni mwa Kundi B.
Nafasi hiyo ilikuja baada ya ushindi wa mechi tatu za awali, hivyo Stars kufikisha pointi 10 na kuingia kwa mara ya kwanza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Kwa upande wao, CAR walishuka dimbani wakiwa tayari wameshaondoshwa kwenye michuano hiyo, ingawa walitaka kuepuka kichapo cha nne mfululizo katika mechi zao dhidi ya Stars.
Katika Kundi B, Madagascar nayo imeingia robo fainali ikiwa nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi saba kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burkina Faso.
Mauritania, ambayo pia ina pointi saba, inashika nafasi ya tatu na imeondoshwa kwa tofuati ya bao moja tu (dhidi ya Madagascar).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img