28.7 C
New York

Wanaume washauriwa kuvaa kaptula ofisini

Published:

TOKYO, Japan

MAMLAKA za Tokyo zimewashauri wafanyakazi wa ofisini kuachana na suti, na badala yake kuvaa kaptula kipindi hiki cha joto kali.

Kwa mujibu wa mamlaka, zinajaribu kuzishawishi kampuni kuwaruhusu wafanyakazi wake kuingia ofisini na kaptula na ‘t-shirt’.

“Tunataka kuwapa watu uhuru zaidi katika kipindi hiki cha ongezeko la joto, bila kupangia watu nini cha kuvaa,” imeeleza taarifa hiyo.

Wakati wengine wakifurahia, wakosoaji wanasema uhuru huo wa mavazi unaondosha utamaduni wa uvaaji katika maeneo ya kazi.

Katika utafiti wa Juni, 2026, asilimia 53.5 ya wadau walieleza kutwaa kuvutiwa na staili hiyo, huku asilimia 46.5 wakieleza kuufurahia.

Related articles

Recent articles