LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI mpya wa Chelsea, Morgan Rogers, atavaa jezi namba 17 msimu ujao, ambayo iliwahi kuvaliwa na lejendari wa timu hiyo, Eden Hazard.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa England amejiunga na Blues akitokea Aston Villa.
Rogers amesaini mkataba utakaombakiza Stamford Bridge hadi mwaka 2033, usajili huo ukiigharimu Chelsea kitita cha Pauni milioni 117.
Kama itakumbukwa, jezi hiyo namba 17 iliwahi kuvaliwa pia na Pedro na Mateo Kovacic.
Kabla ya Rogers kupewa, jezi hiyo ilikuwa ikivaliwa na raia wa Brazil, Andrey Santos, ambaye ametimkia Manchester United.
Santos ametimka Chelsea na kujiunga na ‘Mashetani Wekundu’ kwa ada ya Pauni milioni 50.


