14.7 C
New York

Waziri Mkuu jela miaka 20

Published:

N’DJAMEA, Chad
ALIYEWAHI kuwa Waziri Mkuu wa Chad, Succes Masra, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani akishutumiwa kwa kuchochea ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa kigeni nchini humo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mwanasheria wake, Kadjilembay Francis, kiongozi huyo anayo nafasi ya kukata rufaa.
Masra, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Chad kuanzia Januari hadi Mei, mwaka jana, kwa sasa ni kiongozi wa Chama cha upinzani cha Transformers.
Tangu wakati huo, Masra amekuwa mkosoaji mkubwa wa utendaji wa Serikali inayoongozwa na Rais Mahamat Deby.
Masra na washitakiwa wengine 67 walituhumiwa kwa kuchochea mapigano kati ya wakulima na wafungaji yaliyosababisha vifo vya watu 35.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, mwanasiasa huyo alishika nafasi ya pili, wakati Rais Deby alipoingia Ikulu kwa ushindi wa asilimia 61 ya kura.
Hata hivyo, Masra aligomea matokeo ya Uchaguzi huo kwa kile alichodai kuwa uligubikwa na ‘rafu’ nyingi.
Baadaye, alikubaliana na matokeo, ambapo sasa alipewa nafasi ya kuwa Waziri Mkuu baada ya majadiliano na Rais Deby.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img