14.7 C
New York

UN yaionya Israel kuhusu Gaza

Published:

LOS ANGELES, Marekani
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limeitaka Israel kuacha mara moja mpango wake wa mpya wa ‘kuuteka’ Mji wa Gaza.
Kauli hiyo imetokana na mkutano wa dharura uliofanywa na Baraza hilo ili kujadili mpango wa Israel kutaka kuumiliki Mji wa huo.
Mpango wa Israel, endapo utafanikiwa, utasababisha raia wa Palestina takribani milioni moja kukosa makazi.
Israeli wametangaza mpango huo, huku wakiendeleza mashambulizi katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya Wapalestina 39.
Akizungumza katika Mkutano huo wa UN, Mkuu wa Idara ya masuala ya utu, Ramesh Rajasingham, alisema hatua hiyo ya Israel itaongeza maafa katika Ukanda wa Gaza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img