Na Mwandishi Wetu, Gazetini
KLABU ya Yanga imetangaza rasmi kuwa Mkutano Mkuu wake utafanyika Septemba 7, mwaka huu.
Taarifa rasmi ya Yanga kwa wanachama wake imeweka wazi kuwa Mkutano Mkuu huo utaanza saa 4 asubuhi katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) uliopo Posta jijini Dar es Salaam.
Ifahamike kuwa Mkutano Mkuu huo ni kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya klabu hiyo ya mwaka 2021.
Miongoni mwa ajenda ni kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka kwa Kamati ya Utendaji, pamoja na kusomewa mapato ma matumizi ya klabu.
Wakati huo huo, hotuba ya Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, ni ajenda nyingine ya Mkutano huo, ambao pia utapitisha Bajeti ya klabu kwa mwaka unaofuata.


