Na Mwandishi Wetu
Msanii Nurdin Bilal maarufu Shetta, ameshinda kwenye kura za maoni ya kugombea udiwani Kata ya Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam kupitia CCM.
Katika mchakato huo leo Agosti 4, 2025, Shetta amepata kura 293, Azimkhan Akber Azmkhan kura 178 na Joseph Ngowa akipata kura saba.


