11.6 C
New York

Waandamana kumpinga rais Ukraine

Published:

KYIV, Ukraine

MAELFU ya raia wa Ukraine wameandamana kuipinga hatua ya Rais Volodymyr Zelensky kupitisha sheria inayobana uhuru wa taasisi kubwa mbili, ikiwamo ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Nabu).

Sheria mpya hiyo inaifanya Nabu, pamoja na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka ya Rushwa (Sap), kuwa chini ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, ambaye kimsingi anateuliwa na rais.

Rais Zelensky alisaini muswada huo Jumanne ya wiki hii baada ya kuungwa mkono na wabunge 263 kati ya 324. Pia, kwa upande wake, kiongozi huyo aliikingia kifua sheria mpya akisema taasisi hizo (Nabu na Sap) zimeshindwa kumaliza mashitaka mengi ya rushwa, pia akizitaja kuwa na ‘mkono’ wa Urusi katika utendaji wake.

Lakini, katika maandamano ya siku mbili mjini Kyiv, wananchi wameonekana wakiwa na mabango yenye jumbe zinazoikosoa sheria hiyo. Kutokana na presha iliyopo, Rais Zelensky alikiri kuwa sheria hiyo inapaswa kutazamwa upya, akiahidi kupeleka mswada mpya bungeni.

Wakati huo huo, washirika wa Serikali ya Ukraine nao wameeleza kutokuvutiwa na sheria hiyo.
Mathalan, Msemaji wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, alisema ameomba maelezo ya kina kutoka kwa Serikali ya Ukraine.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img