MERSEYSIDE, England
KLABU tajiri ya Al-Nassr ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia imemtengea dau nono winga wa Liverpool, Luis Diaz.
Taarifa zinaeleza kuwa Al-Nassr itaipelekea Liver ofa ya euro milioni 100 (zaidi ya Sh bil. 360 za Tanzania).
Diaz mwenye umri wa miaka 28, alijiunga na Liver mwaka 2022 akitokea FC Porto na mkataba wake umebakiza miezi 24.
Msimu uliopita, nyota huyo raia wa Colombia alicheza mechi 50, ambapo alifunga mabao 17 na kutoa ‘asisti’ nane.


