19.5 C
New York

Makocha waliotimuliwa wakiwa na siku chache kazini

Published:

LONDON, Uingereza
MWEZI uliopita, Ange Postecoglou aliweka rekodi ya kuwa kocha aliyefukuzwa ndani ya muda mfupi zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England (EPL).
Mabosi wa Nottingham Forest walimtimua akiwa amefanya kazi kwa siku 39 tu tangu alipotangazwa kuwa kocha wa klabu hiyo.
Les Reed (Siku 41)
Charlton ilimtangaza kuwa kocha baada ya klabu hiyo kumfuta kazi mwishoni mwa mwaka 2004. Reed alidumu kwenye nafasi hiyo kwa wiki sita tu.
Wakati huo Charlton ikiwa Ligi Kuu ya England, ilimtimua baada ya kushinda mechi moja na kutolewa katika michuano ya Kombe la Ligi (sasa Carabao Cup).
Rene Meulensteen (siku 75)
Mholanzi huyo aliinoa Manchester United kwa miaka sita, kisha akaajiriwa na Anzhi Makhachkala ya Ligi Kuu ya Urusi.
Hata hivyo, Fulham ilimng’oa Urusi na kumrejesha Ligi Kuu ya England mwaka 2023, akichukua nafasi ya Martin Jol, lakini alifukuzwa akiwa ameiongoza katika mechi 13 tu.
Frank de Boer (siku 77)
Wakati wa majira ya kiangazi mwaka 2017, Crystal Palace walikuwa njiapanda juu ya ni kocha yupi angewafaa kati ya Roy Hodgson na Frank de Boer.
Walichagua kumpa ajira De Boer, ambaye wakati huo alikuwa ametoka kuachana na Inter Milan ya Serie A.
Hata hivyo, Palace waliuanza msimu kwa kupoteza mechi nne mfululizo bila kufunga bao na Mholanzi huyo akatimuliwa akiwa amefanya kazi siku 77 tu.
Bob Bradley (siku 84)
Mwaka 2016, Bradley aliandika historia ya kuwa kocha wa kwanza raia wa Marekani kufanya kazi England. Aliajiriwa na klabu ya Swansea.
Hata hivyo, baada ya kuambulia pointi nane pekee katika mechi 11 za Ligi Kuu, mabosi wa Swansea waliona inatosha na kumtimua kwenye benchi la ufundi.
Quique Sanchez Flores (siku 85)
Akiwa na historia ya kuinoa Watford mwaka 2016, kocha huyo raia wa Hispania alirejea klabuni hapo miaka mitatu baadaye.
Tofauti na mwaka 2016, ambapo aliweza hata kupata tuzo Kocha Bora wa Mwezi, Flores alishia kufukuzwa akiwa ameinoa timu hiyo kwa siku 85 tu.
Terry Connor (siku 91)
Baada ya mabosi wa Wolves kukubaliana juu ya kumfuta kazi Mick McCarthy mwaka 2012, walimpa jukumu hilo aliyekuwa msaidizi wake, Terry Connor.
Hata hivyo, licha ya kuanza na sare dhidi ya Wolves, Connor alipoteza mechi saba mfululizo zilizofuata. Akafungashiwa virago.

Related articles

Recent articles