HOUSTON, Marekani
KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Ureno, Roberto Martinez, haoni kama ni sahihi kwa nahodha wake, Cristiano Ronaldo, kukosolewa baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya DRC.
Ronaldo alimaliza dakika zote 90, ingawa wengi waliamini angestahili kutolewa kutokana na kiwango chake kibovu katika mechi hiyo ya Kombe la Dunia.
Wachambuzi wa soka kadhaa si tu walikosoa, bali pia walisema uwepo wake uwanjani uliifanya timu ikose ubora.
Akijibu, Martinez amesema hakuona sababu ya kumtoa staa huyo, licha ya kwamba ni kweli hakuwa kwenye ubora wake.
“Haikuwa na maana yoyote kumtoa Cristiano Ronaldo, ambaye ni mfungaji bora kwenye histroria,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.
Je, Ronaldo atawaziba mdomo wakosoaji wake katika mchezo wao wa pili dhidi ya Uzbekistan?


