25.4 C
New York

Lionel Messi agoma…

Published:

NEW YORK, Marekani

NAHODHA wa kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi, amesema alijikuta akilia baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Algeria.

Hata hivyo, supastaa huyo wa kandanda hajaeleza kilichomliza, na badala yake amesema ni ‘ishu’ binafsi.

Katika mchezo huo wa kwanza, Messi mwenye umri wa miaka 38, aliongeza mengine mawili, hivyo kumaliza akiwa na ‘hat-trick’.

“Nililia baada ya bao la kwanza, ndiyo. Lakini ni masuala binafsi, hayahusiani na soka,” amesema nyota huyo wa Inter Miami ya Marekani.

Messi ameeleza kuwa alipitia nyakati ngumu lakini wachezaji wenzake walikuwa naye bega kwa bega kuhakikisha anakaa sawa.

Related articles

Recent articles