20.5 C
New York

Hakimi aandika historia mpya Kombe la Dunia

Published:

MEXICO CITY, Mexico

NAHODHA wa timu ya soka ya Morocco, Achraf Hakimi, amekuwa mchezaji wa Afrika aliyecheza mechi nyingi za Kombe la Dunia.

Nyota huyo wa PSG ameandika historia hiyo baada ya kufikisha michezo 12 za michuano hiyo akiwa na kikosi cha Morocco.

Hakimi alifikisha idadi hiyo katika mchezo dhidi ya Scotland, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia, Brazil.

Hakimi (27), anawapiku mechi moja Francois Omam-Biyik wa Cameroon na Asamoah Gyan wa Ghana, ambao walistaafu kwa nyakati tofauti wakiwa na michezo 11 ya mashindano hayo.

Nyota huyo ameshiriki mara tatu fainali za Kombe la Dunia na kucheza mechi zote.

Related articles

Recent articles