BRUSSELS, Ubelgiji
LICHA ya kutokuwa na taji kubwa, Ubelgiji ni moja ya mataifa yanayofanya vizuri katika ulimwengu wa soka. Nafasi ya nane kwenye viwango vya ubora duniani.
‘Red Devils’ iliishia hatua ya makundi msimu uliopita wa Kombe la Dunia, ikiwa ni mara ya kwanza kutolewa mapema kwenye michuano hiyo tangu mwaka 1998.
Ni baada ya aibu hiyo, kocha Roberto Martinez aliwajibishwa kwa kufukuzwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Rudi Garcia aliyeajiriwa Januari, mwaka huu.
Katika mechi za kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia, kiungo wake, Kevin De Bruyne, alifanya kazi kubwa ya kufunga mabao sita.
Hata hivyo, ukiacha staa huyo wa Napoli, kikosi hicho kina mastaa wengine, wakiwamo Youri Tielemans (Aston Villa) na Jeremy Doku (Manchester City).
Wakati huo huo, Ubelgiji inaye mfungaji bora wake wa muda wote, Romelu Lukaku, ingawa majeraha ya paja yamemzuia kuitumikia Napoli tangu msimu huu uanze.
Ubelgiji inarejea Kombe la Dunia baada ya kuishia makundi msimu uliopita, ambapo ilikuwa Kundi moja na Morocco, Croatia na Canada.
Je, kocha Garcia atafanya maajabu katika awamu ya 15 ya ushiriki wao kwenye michuano hiyo ya FIFA?
Published:


