6.4 C
New York

WHO: Wanawake milioni 840 wamepitia unyanyasaji wa kijinsia

Published:

NEY YORK, Marekani
RIPOTI mpya ya Shirika la Afya ya Umoja wa Mataifa (WHO) imeeleza kuwa kati ya wanawake watatu, basi mmoja atakuwa amewahi kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia.
Kupitia ripoti hiyo inayotokana na utafiti katika mataifa 168 kuanzia mwaka 2000 hadi 2023, wastani huo ni sawa na wanawake milioni 840 duniani.
Aidha, inaeleza kuwa wanawake milioni 316 na wasichana wenye umri wa miaka 15 walifanyiwa hivyo na watu wao wa karibu.
“Unyanyasaji wa wanawake ni moja ya uvunjifu mkubwa wa haki na wa miaka mingi na bado unaendelea,” amesema Mkurugezi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Wakati huo huo, amesema kutokana na takwimu hizo, hakuna jamii iliyo salama linapokuja suala la unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.
“Hakuna jamii inayoweza kusema iko salama ikiwa nusu ya watu wake wanaishi kwa hofu.
“Kumaliza tatizo hili siyo tu kwa kuandaa sera, bali ni suala la utu, usawa na haki za binadamu,” amesisitiza Ghebreyesus.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img