RABAT, Morocco
PYRAMIDS FC ya Ligi Kuu nchini Misri imetwaa tuzo ya Klabu Bora Afrika kwa mwaka huu, ikiipiku Simba SC ya Tanzania.
Mbali ya Simba, baadhi ya klabu zingine zilizokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni CR Belouizdad, Orlando Pirates, Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas, Al Hilal na RS Berkane.
Simba ‘Wekundu wa Msimbazi’ waliingia kwenye mchuano huo kutokana na mafanikio yao ya msimu uliopita, ambapo walifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa upande wao, Pyramids wametangazwa kuwa washindi kwa mafanikio yao ya kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa Afrika na CAF Super Cup msimu uliopita.
Ikumbukwe, vigogo hao wa Cairo waliing’oa Orlando Pirates katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika.
Katika mchezo wa fainali, Pyramids waliifunga timu nyingine kubwa kutoka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.
Baadaye, ilitwaa taji la CAF Super Cup kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wakali wa Ligi Kuu ya Morocco, RS Berkane.
Published:


