19.2 C
New York

Renard apewa mikoba ya kocha Tunisia

Published:

MEXICO CITY, Mexico

SHIRIKISHO la Soka la Tunisia limemtangaza Herve Renard kuwa kocha mpya wa timu yake ya Taifa.

Renard (57), amepewa ajira hiyo akichukua nafasi ya Sabri Lamouchi aliyefukuzwa baada ya Tunisia kufungwa mabao 5-1 na Sweden katika mchezo wa kwanza wa Kundi F msimu huu wa Kombe la Dunia.

Kocha huyo, Renard, alikuwa na kikosi cha Morocco katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018, kabla ya kuiongoza Saudi Arabia (2022).

Hata hivyo, Mfaransa huyo amekuwa nje ya kazi tangu Aprili, 2026, baada ya kufukuwa katika benchi la ufundi la Saudia.

Mwaka 2023, Renard alikuwa kwenye benchi la ufundi la timu ya soka ya Wanawake ya Ufaransa iliyoshiriki Kombe la Dunia.

Related articles

Recent articles