20.9 C
New York

Pogba atoa neno kuhusu Yamal

Published:

PARIS, Ufaransa

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba, amemtaja Lamine Yamal wa Barcelona katika orodha yake ya wachezaji bora watano duniani.

Pogba amayesema hayo muda mfupi baada ya Hispania kulazimishwa suluhu na Cape Verde katika mchezo wa jana wa hatua ya makundi msimu huu wa Kombe la Dunia.

Yamal (18), amekuwa na mchango mkubwa si tu kwa Barcelona, bali pia kwenye kikosi cha Hispania.

Msimu uliopita, aliiongoza Barcelona kutwaa kwa mara ya pili mfululizo taji la Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).

Mwaka 2025, kinda huyo alishika nafasi ya pili, nyuma ya Ousmane Dembele, katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mchezaji Bora ya Ballon d’Or.

“Hata kama si mchezaji bora zaidi, yupo kwenye wale watatu bora duniani kwa sasa,” amesema Pogba.

“Ningemshauri Lamine acheze soka tu, aachane na mambo mengine. Anapaswa kuwa na watu sahihi – familia na wakala wake.”

Related articles

Recent articles