NEW YORK, Marekani
BAADA ya kufukuzwa katika benchi la ufundi la timu ya soka ya Tunisia, Sabri Lamouchi hajawa kocha wa kwanza kutimuliwa mapema katika historia ya Kombe la Dunia.
Lamouchi alifungashiwa virago baada ya Tunisia kufungwa mabao 5-1 katika mechi ya kwanza msimu huu wa fainali hizo za FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).
CARLOS ALBERTO (1998)
Michuano ilifanyika Ufaransa na timu ya soka ya Saudi Arabia ilipoteza mechi yake ya kwanza kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Denmark.
Kocha Alberto alifukuzwa baada ya mchezo huo. Alipoondoka, Saudia ikapata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Korea Kusini na safari yao ikaishia hatua ya makundi.
CHA BUM-KUN (1998)
Alifukuzwa baada ya Korea Kusini kupoteza mechi zote mbili za kwanza, ikiruhusu jumla ya mabao nane mbele ya Mexico na Uholanzi.
Baadaye, Bum-kun alitupa lawama kwa Chama cha Soka cha Korea akisema wachezaji walikuwa wanadai posho zao, pia mechi za Ligi Kuu nchini humo zilikuwa na upangaji wa matokeo. Alifungiwa miaka mitano kujihusisha na soka.
HENRYK KASPERCZAK (1998)
Tunisia waliingia katika fainali hizo wakiwa na morali kubwa baada ya kufanya vizuri mwaka 1994 nchini Argentina.
Baada ya kupoteza mechi mbili za mwanzo dhidi ya England (2-0) na Colombia (1-0) walimtimua Kasperczak, kisha wakapata sare (1-1) dhidi ya Romania na safari yao kuishia hapo.


