20.3 C
New York

Mazito yafichuka ‘urafiki’ wa M23, Rwanda

Published:

NAIROBI, Kenya

RWANDA inashirikiana kwa karibu na wapiganaji wa M23 kuteka raia, hasa vijana na watoto, na kuwaingiza katika kundi hilo linalopigana na wanajeshi wa Serikali nchini DRC.

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu la Human Right Wach (HRW) katika ripoti yake ya hivi karibuni, operesheni hiyo ya kulazimishwa kujiunga na M23 inawakuta pia wanajeshi wa Serikali ya DRC wanaotekwa.

Katika ripoti yake ya kurasa 78, HRW imeeleza kuwa maeneo ya Mashariki mwa DRC ndiyo kitovu cha operesheni hiyo, ambapo maelfu ya raia na wanajeshi wa DRC wako chini ya M23.

Utafiti wa Shirika hilo umebaini kuwa wanajeshi wa Rwanda na M23 wanashikilia maelfu ya raia katika kambi za mafunzo za Rumangabo na Tshanzu zilizopo mkoani Kivu.

“M23 inayoungwa mkono na Rwanda inaendesha kile inachokiita kambi za mafunzo huko Mashariki mwa DRC, ambapo raia wanaochukuliwa wamekuwa wakiteswa,” anasema mmoja ya watafiti wa HRW, Clementine de Montjoye.

Baadhi ya mateso hayo ni pamoja na kupigwa, kunyimwa chakula, maji, dawa/tiba, na unyanyasaji wa kingono, ikiwamo kubakwa.

“Ukikutwa unakunywa maji bila ruhusa, walinzi wanakupiga,” anasema raia aliyewahi kutekwa na kushikiliwa kwa miezi mitano na M23.

Anasisitiza kuwa kinachoendelea kati ya Rwanda na M23 ni uhalifu wa kivita unaopaswa kuchunguzwa ili pande mbili hizo zifunguliwe mashitaka.

Licha ya shutuma za miaka mingi, kwamba Serikali ya Rwanda inafanya kazi kwa karibu na M23, Taifa hilo limeendelea kukanusha na kuziita taarifa hizo kuwa ni ‘porojo za kisiasa’.

Related articles

Recent articles