CATALUNYA, Hispania
KLABU ya Barcelona inaangalia uwezekano wa kuiambia Manchester United imchukue mshambuliaji wake raia wa England, Marcus Rashford.
Rashford alijiunga na Barcelona kwa mkopo akitokea Man United, dili hilo likigharimu kitita cha Pauni milioni 30.
Klabu hiyo ya La Liga ilimgeukia ghafla staa huyo baada ya kuwakosa Luis Diaz na Nico Williams.
Licha ya kuonesha kiwango kizuri wakati wa maandalizi ya msimu (pre-season), Rashford hajafunga bao wala kutoa ‘asisti’ katika mechi tatu za msimu huu wa La Liga.
Kutokana na kusuasua kwa kiwango chake, mabosi wa Barca wameanza kufikiria uwezekano wa kumrudisha Old Trafford.
Taarifa zinaeleza kuwa Rais wa klabu, Joan Laporta, na Mkurugenzi wa Michezo, Deco, hawavutiwi na kiwango cha mchezaji huyo.
Hata hivyo, endapo Barcelona wataamua kumrudisha, basi watalazimika kuilipa Man United kiasi cha Pauni milioni 4.3.
Published:


