9.8 C
New York

Guardiola afunguka kilichoiponza City kwa Brighton

Published:

MANCHESTER, Uingereza
BAADA ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Brighton, kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ameeleza sababu ya kupoteza mchezo huo wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Brighton ilipata mabao yake kupitia kwa kiungo wa zamani wa Man City, James Milner, na Brajan Gruda aliyetokea benchi na kufunga katika dakika ya 89 ya mtanange huo.
Kwa bao hilo la mkwaju wa penalti katika dakika ya 67, Milner amekuwa mchezaji wa pili mwenye umri mkubwa kufunga bao katika historia ya EPL.
Ushindi huo ulikuja licha ya Man City kuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Erling Haaland, akifikisha mabao 100 ya Ligi Kuu.
Alipoulizwa sababu ya kupoteza mchezo baada ya kuongoza, Guardiola alisema penalti ya Milner ilibadili mchezo na kuifanya Man City ishindwe kucheza katika kiwango kizuri ilichoanza nacho mchezo.
“Ni kweli wakati mwingine mambo hubadilika baada ya kuruhusu bao, lakini tulipoteza aina yetu ya uchezaji. Tuliacha kucheza kama tulivyokuwa saa moja kabla ya penalti,” alisema.
Kichapo hicho ni cha pili mfululizo kwa Man City baada ya kile cha mabao 2-0 kutoka kwa Tottenham siku chache zilipita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img