15.5 C
New York

Rais Indonesia aibuka, alaani maandamano

Published:

JAKARTA, Indonesia
RAIS wa Indonesia, Prabowo Subianto, ameyaita kuwa ni uhaini na ugaidi maandamano ya raia yanayoendelea nchini humo.
Indonesia, Taifa la Kusini-Mashariki mwa Asia, inakabiliwa na maandamano ya raia wanaokwaza na kupanda kwa gharama za maisha.
Aidha, maandamano hayo yameripotiwa kuongezeka baada ya kifo cha dereva wa usafiri wa ‘taxi’ aliyekuwa akikimbizwa na gari la polisi.
Wakati huo huo, maandamano hayo yaliishuhudia raia wakifika na kufanya uharibifu mkubwa nyumbani kwa Waziri wa Fedha, Sri Mulyani Indrawati.
Akizungumzia hali ilivyo, Rais Subianto alisema licha ya kwamba maandamano ni haki ya raia, bado kumekuwapo na ukiukwaji mkubwa wa sheria.
“Hatuwezi kukataa kuwa kumekuwa na viashiria vya ukiukwaji wa sheria, sawa na uhaini na ugaidi,” alisema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img