9.8 C
New York

Mainoo apigwa ‘stop’ kuondoka United

Published:

MANCHESTER, Uingereza
LICHA ya Kobbie Mainoo kuomba kuondoka kwa mkopo, Manchester United imemwambia kiungo huyo abaki na kuipambania namba kikosini.
Kwa sasa, klabu kadhaa za Ulaya zimeonesha nia ya kumsajili nyota huyo, ikiwamo Napoli ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A).
Akizungumza hivi karibuni, kocha wa Man United, Ruben Amorim, alisema anataka kuona Mainoo akibaki Old Trafford.
“Nataka Kobbie abaki. Anapaswa kuipambania namba yake, tunamuhitaji Kobbie. Naamini mambo yatabadilika,” alisema.
Mainoo mwenye umri wa miaka 20, alicheza dakika zote 90 katika mchezo uliopita wa Kombe la Ligi dhidi ya Grimsby Town.
Kabla ya hapo, kinda huyo aliishia benchi katika mechi zote mbili za Ligi Kuu, nafasi yake akicheza Bruno Fernandes.
Kwa upande mwingine, nyota huyo wa kimataifa wa England ana mkataba na Man United utakaofikia ukomo mwaka 2027.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img