LONDON, Uingereza
KLABU ya Tottenham iko kwenye hatua nzuri ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Uholanzi, Xavi Simons.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Tottenham wamefikia hatua hiyo baada ya kukubali kuweka mezani kiasi cha Pauni milioni 51.8.
Taarifa zinaeleza kuwa Simons ameshatua Kaskazini mwa Jiji la London kwa ajili ya zoezi la kufanyiwa vipimo.
Chelsea ilikuwa ya kwanza kumtaka Simons, ikielezwa kuwa ilikutana mezani na mabosi wa Leipzig mwanzoni mwa majira haya ya kiangazi.
Hata hivyo, Blues waliamua kuachana na usajili huo na badala yake kumsajili Alejandro Garnacho kutoka Manchester United.
Simons anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Tottenham kipindi hiki baada ya klabu hiyo kuzinasa saini za Joao Palhinha na Mohammed Kudus.
Published:


