9.8 C
New York

Alexander-Arnold, Grealish waachwa kikosini England

Published:

LONDON, Uingereza
KOCHA wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel, hajamjumuhisha beki Trent Alexander-Arnold katika kikosi kitakachocheza mechi mbili za kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Wakati huo huo, kocha Tuchel hajamwita winga wa Everton, Jack Grealish, licha ya kiwango chake kizuri katika mchezo uliopita dhidi ya Brighton.
England ‘Three Lions’ inajiwinda kuzikabili Andorra na Serbia, ikiwa ni katika kusaka tiketi ya kushiriki fainali hizo za mwakani.
Mlinzi wa kulia huyo mwenye umri wa miaka 26, aliondoka Liverpool na kutimkia Real Madrid wakati huu wa usajili wa majira ya kiangazi.
Wikiendi iliyopita, Alexander-Arnold hakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Real Madrid katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Real Oviedo.
Wakati huo huo, Tuchel amemwita kwa mara ya kwanza kiungo wa Nottingham Forest, Anderson.
Licha ya kurejea kwa Marcus Rashford, Adam Wharton na Jordan Henderson, kikosi hicho kinawakosa pia Jude Bellingham, Bukayo Saka, Cole Palmer na Levi Colwill, ambao wanauguza majeraha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img