MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema timu yake ilipoteza dira ndani ya uwanja na hiyo ikasababisha itolewe kwenye michuano ya Carabao Cup.
Man United ilitolewa kwenye mashindano hayo usiku wa jana baada ya kichapo cha penalti 12-11 kutoka kwa ‘vibonde’ Grimsby Town.
Mchezo huo, ambao ulishuhudia Amorim akifanya mabadiliko nane katika kikosi kilichoivaa Fulham, ulifika kwenye mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Staa mpya wa Man United, Matheus Cunha, ndiye aliyekosa penalti iliyohitimisha safari yao mbele ya timu hiyo ya madara ya chini.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Amorim alisema: “Tulianza mchezo bila kasi, tukapotea. Nafiriki timu bora ndani ya uwanja ndiyo iliyoshinda. Tunapaswa kubadilika sasa.”
Man United, mabingwa mara 20 wa taji la Ligi Kuu (EPL), walimaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo. Ni nafasi mbaya zaidi tangu mwaka 1974.
Published:


