MADRID, Hispania
VIGOGO wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Real Madrid, wanaipigia hesabu saini ya kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo.
Madrid sasa inaungana na Atletico Madrid na klabu nyingi za Ulaya zinazomtolea macho nyota huyo aliyepoteza namba kwenye kikosi cha kocha Ruben Amorim.
Mainoo (20), ambaye aliibuka akitokea katika ‘academy’ ya Old Trafford, hajacheza hata dakika moja tangu msimu huu wa Ligi Kuu ya England uanze.
Kwa upande mwingine, Mainoo si mchezaji pekee anayehusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford majira haya ya kiangazi.
Winga raia wa Argentina, Alejandro Garnacho, ameshaambiwa atafute maisha mapya nje ya klabu hiyo, ambapo kwa sasa anahusishwa na matajiri wa London, Chelsea, wanaotaka kumsajili kwa Pauni milioni 35.
Published:


