9.8 C
New York

Vardy kumalizia soka Serie A?

Published:

MILAN, Italia
BAADA ya kuachwa na Leicester City, huenda Jamie Vardy akajiunga na moja ya klabu za Ligi Kuu ya Italia (Serie A).
Vardy (38), kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuiacha Leicester aliyokuwa ameifungia mabao 200 katika mechi 500.
Nyota huyo ametajwa kuwa kwenye mazungumzo na timu mpya Serie A, Cremonese, ambayo iliifunga AC Milan mabao 2-1 wikiendi iliyopita.
Awali, Vardy alikaribia kujiunga na Genoa lakini kocha wa timu hiyo, Patrick Vieira, aliupinga usajili huo.
Katika taarifa nyingine, Vardy ameripotiwa kuvutiwa zaidi na mpango wa kumfuata kocha wake wa zamani, Brendan Rodgers, ambaye anainoa Celtic.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img