14.7 C
New York

Fernandes awindwa Saudi Arabia

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KLABU tajiri ya Al-Ittihad iko mstari wa mbele kuiwania saini ya staa wa Manchester United, Bruno Fernandes, ikipanga kumnasa wakati huu wa usajili wa majira ya kiangazi.
Kwa mujibu wa taarifa, tayari mabosi wa Al-Ittihad ya Saudi Arabia wameshakutana na kufanya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno.
Hii ni mara ya pili kwa Fernandes kuhusishwa na Ligi Kuu ya Saudia, ikikumbukwa kuwa Al-Hilal na Al-Nassr nazo zilitajwa kumtolea macho.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kocha wa Al-Nassr, Jorge Jesus, ambaye pia ni Mreno, nyota huyo hana mpango wa kuondoka Old Trafford.
“Nilitaka kumsajili, lakini Bruno anataka kubaki (Man United. Nilizungumza naye mwaka jana, alisema anataka kubaki,” alisema Jesus.
Kwa upande mwingine, Fernandes anataka mshahara wa si chini ya Pauni milioni 33 kwa mwaka endapo ataamua kuipa kisogo Man United.
Wakati fulani, naye aligusia kuwa hana mpango wa kuondoka Man United. “Nilishasema, nipo hapa mpaka klabu itakaponiambia niondoke …” alisema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img