LOS ANGELES, Marekani
BINGWA wa dunia mara mbili kwa upande wa tenesi, Venus Williams, amesema mapenzi yake kwa mchezo huo ndiyo sababu ya kuamua kushiriki US Open akiwa na umri wa miaka 45.
Mwanzoni mwa mwaka huu, zilikuwepo tetesi nyingi zikimuhusisha Venus na mpango wa kuachana na tenesi kutokana na umri wake.
Hata hivyo, sasa nyota huyo raia wa Marekani anajiandaa kushiriki US Open kwa mara ya 25 na kesho atamvaa Karolina Muchova wa Czech.
“Ni furaha iliyoje kuona nimerudi. Si suala la umri, ni suala la namna nilivyofurahi,” alisema Venus, ambaye ana mataji makubwa saba.
Baada ya kuwa nje ya mashindano kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja, bibiye huyo aliibukia Washington Open lakini aliishia raundi ya pili.
Alipomfunga Peyton Stearns katika raundi ya kwanza, alivunja rekodi ya miaka 21 ya kuwa kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa kupata ushindi katika mechi ya michuano ya wanawake.
Published:


