14.7 C
New York

De Bruyne, McTominay waongoza ‘mauaji’ Napoli

Published:

NAPOLI, Italia
KIUNGO wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne, alifunga bao la pili, baada ya Scott McTominay kuitanguliza Napoli, mchezo wa Serie A uliomalizika kwa Napoli kushinda mabao 2-0 dhidi ya Sassuolo.
De Bruyne (34), alifunga ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu alipojiunga na Napoli akitokea kwa matajiri wa England, Manchester City.
McTominay, nyota wa zamani wa Manchester United, aliitanguliza Napoli kwa bao la dakika ya 17, akiunganisha kwa kichwa krosi ya winga raia wa Italia, Matteo Politano.
McTominay (28), amefikisha mabao 12 katika mechi 34 za Ligi Kuu hiyo ya Italia tangu aliposajiliwa na Napoli akitokea Man United mwaka 2024.
Msimu uliopita, nyota huyo alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Serie A baada ya kuiongoza Napoli kutwaa taji hilo. Ni miongoni mwa wanaowania tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.
Katika mchezo mwingine wa Serie A, Genoa na Lecce zilimaliza dakika 90 kwa kugawana pointi baada ya matokeo ya suluhu (0-0).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img