MUNICH, Ujerumani
KOCHA wa zamani wa Manchester United, Erik ten Hag, amepoteza mechi yake ya kwanza ya Bundesliga akiwa kocha wa Bayer Leverkusen.
Leverkusen walianza vizuri mchezo huo kwa bao la mapema la Jarell Quansah lakini wapinzani wao, Hoffenheim, walisawazisha kupitia kwa Fisnik Asllani.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Hoffenheim walirudi kwenye nyavu za Leverkusen kwa bao la ushindi lililopachikwa na Tim Lemperle aliyetumia ‘asisti’ ya Quansah.
Leverkusen walimaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya pili, wakizidiwa pointi 13 na mabingwa Bayern Munich.
Katika mchezo mwingine, Borussia Dortmund waliobaki 10 uwanjani baada ya Filippo Mane kulimwa kadi nyekundu dakika ya 85 walilazimishwa sare ya mabao 3-3 na St Pauli.
Kiungo mpya wa Dortmund, Jobe Bellingham, alicheza mechi yake ya kwanza ya Bundesliga tangu aliposajiliwa majira haya ya kiangazi akitokea Sunderland.
Published:


