14.7 C
New York

Bailey aandika historia Serie A

Published:

ROMA, Italia
BAADA ya kujiunga na AS Roma, winga aliyekuwa Aston Villa, Leon Bailey, anakuwa mchezaji wa kwanza raia wa Jamaica kuitumikia klabu hiyo ya Serie A.
Bailey ametua AS Roma kwa mkopo wa euro milioni 2, ingawa wanaweza kumsajili moja kwa moja endapo watavutiwa naye.
Nyota huyo alizaliwa Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Kingston, na alitimkia Ulaya akiwa na umri wa miaka 13, akicheza soka Ubelgiji, Ujerumani na England.
Akiwa KFC Genk ya Ubelgiji aliyojiunga nayo mwaka 2015, Bailey alifunga mabao 15 katika mechi 77.
Alitua Bundesliga mwanzoni mwa mwaka 2017, ambapo alisajiliwa na Bayer Leverkusen.
Kiwango chake akiwa Bundesliga kilimpa nafasi ya kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya Jamaica mwaka 2019.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img