MANCHESTER, England
STAA mpya wa Manchester City, Tijjani Reijnders, amekuwa mchezaji wa kwanza wa klabu hiyo baada ya Sergio Aguero kufunga na kutoa ‘asisti’ katika mechi yake ya kwanza Ligi Kuu ya England (EPL).
Reijnders aliyesajiliwa majira haya ya kiangazi akitokea AC Milan, alihusika katika mabao mawili jana, wakati Man City ilipoichapa Wolves 4-0.
Msimu uliopita, nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye Man City wamemsajili kwa Pauni milioni 46, alitwaa tuzo ya Kiungo Bora wa Serie A, akifunga mabao 10.
Wikiendi iliyopita, Reijnders aliingia kambani mara mbili wakati Man City ilipoitandika Palermo mabao 3-0 katika mchezo wa ‘pre-season’.
Kutokana na namna alivyoichachafya Wolves, ‘mido’ huyo aliondoka na tuzo ya Nyota wa mchezo. “Ni mwanzo mzuri, nimefurahi kufunga na kutoa asisti na ushindi pia,” alisema Reijnders.
Published:


