MANCHESTER, England
RIPOTI zinaeleza kuwa Manchester City wmaebakiza hatua chache tu kukamilisha usajili wa kipa wa PSG raia wa Italia, Gianluigi Donnaruma.
Man City wamehamishia nguvu kwa Donnaruma baada ya kipa wao, Ederson, kuonesha nia ya kuondoka majira haya ya kiangazi.
Matajiri wa soka la Uturuki, Galatasaray, wameshawasilisha ofa yao kwa kipa huyo wa kimataifa wa Brazil.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo mwenye jina kubwa Italia, Fabrizio Romano, Galatasaray wameweka mezani ofa ya Pauni milioni 8.5.
Awali, Man City walieleza wazi kuwa hawana mpango wa kumwachia kipa wao huyo, hasa wakati klabu za Saudi Arabia zilipoonesha nia ya kumsajili mwaka jana.
Lakini, baada ya ofa ya Galatasaray, Man City wamebadili uamuzi na sasa wako tayari kumfungulia mlango wa kutokea pale Etihad.
Published:


