12.6 C
New York

Mechi moja tu, mashabiki hawamtaki kocha West Ham

Published:

LONDON, England
BAADA ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Sunderland katika mechi yao ya kwanza msimu huu wa Ligi Kuu ya England, mashabiki wa West Ham wanataka kocha Graham Potter afukuzwe.
Sunderland iliyorejea Ligi Kuu ikitokea Championship, ilipata mabao yote kipindi cha pili kupitia kwa Eliezer Mayenda, Daniel Ballard na Wilson Isidor.
Kupitia mitandao ya kijamii, mashabiki wa West Ham walieleza kusikitishwa na matokeo hayo, wengine wakisema Potter hawezi kuwapeleka kokote msimu huu.
“Potter anapaswa kuondoka usiku huu, ni mwanzo mbaya sana,” alisema mmoja ya mashabiki hao huko mitandaoni.
Mwingine aliongeza: “Kwa kweli, sioni kama Graham Potter ana ubavu wa kumaliza msimu akiwa hata katikati ya msimamo wa Ligi.”
Kwa upande wake, mwingine alisema: “Graham Potter atimuliwe leo (jana). Hajui hata namna ya kumaliza tatizo la timu. Ni aibu sana hii.”
Aidha, mwingine alienda mbali zaidi na kusema Potter si kocha wa viwango vya Ligi Kuu ya England, hivyo hawezi kuisaidia West Ham.
Tangu Potter alipoajiriwa kuliongoza benchi la ufundi, West Ham imeshinda mechi tano tu kati ya 19 za Ligi ilizocheza chini yake.
Wastani wake wa kushinda mechi ni mdogo (25%) kuliko kocha yeyote katika historia ya West Ham.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img