PARIS, Ufaransa
KLABU kongwe za England, Arsenal na Manchester United, zinapigana vikumbo kuiwania saini ya mshambuliaji wa PSG raia wa Korea Kusini, Lee Kang-in.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alianzia soka katika klabu ya Valencia, akapita Mallorca, kabla ya kutua PSG mwaka 2023.
Kwa miaka miwili klabuni hapo, Kang-in amefunga mabao 13 na kutoa ‘asisti’ 11 katika mechi 86 za mashindano mbalimbali.
Msimu uliopita, aliingia kambani mara sita na kutoa asisti sita katika michezo yake 30 ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), pia akitumika mara 11 kwenye Ligi ya Mabingwa.
Licha ya mkataba wake wa sasa kubakiza miaka mitatu, Arsenal na Man United zinajaribu kuishawishi PSG imwachie majira haya ya kiangazi.
Kwa mujibu wa mtandao wa CaughtOffside, Man United iko mstari wa mbele zaidi kumfukuzia, licha ya kwamba Napoli nayo imeonesha kumtaka.
Published:


