12.6 C
New York

Arteta amjibu mkongwe Arsenal

Published:

LONDON, England
KOCHA Mikel Arteta amesema hana mpango wa kumpokonya unahodha kiungo wake raia wa Noray, Martin Odegaard.
Arteta ni kama amemjibu lejendari wa Arsenal, Tony Adams, ambaye alisema Odegaard hastahili kitambaa cha unahodha.
Katika maoni yake, Adam aliyekuwa akicheza eneo la beki wa kati, Declan Rice ndiye anayepaswa kuwa nahodha wa Arsenal msimu huu.
Kwa mujibu wa Adams, Odegaard amekuwa akikosekana mara kwa mara kikosini, tofauti na Rice anayecheza mechi nyingi zaidi.
“Unahitaji mtu ambaye anapatikana mara zote, ambaye anawashawishi mashabiki kuja uwanjani kumtazama. Huo ndiyo msingi wa timu inayotaka ubingwa,” alisema Adams.
Arteta, kwa upande wake, alisema haoni sababu ya kubadilisha nahodha, isitoshe pia Odegaard anakubalika kwa wachezaji wenzake.
“Niliwaomba wachezaji wapige kura kuchagua nahodha. Kila mmoja alimchagua Martin Odegaard. Jambo muhimu ni mchezaji wanayeamini anastahili kuwaongoza,” alisema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img