15 C
New York

Bondia afariki baada ya kupigwa ‘KO’

Published:

TOKYO, Japan
BONDIA raia wa Japan, Hiromasa Urakawa, amepoteza maisha ikiwa ni wiki moja tu tangu alipopoteza pambano lake kwa ‘KO’ mbele ya Yoji Saito.
Pambano hilo la Agosti 2 mjini Tokyo lilimalizika baada ya Hiromasa mwenye umri wa miaka 28 kupigwa katika raundi ya nane.
Baada ya pambano, Hiromasa alifanyiwa upasuaji wa kuondosha damu iliyokuwa imevuja kwenye ubongo.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Japan kutangaza vifo vya mabondia waliotoka kupoteza ndani ya ulingo.
Kabla ya Hiromasa, Shigetoshi Kotari aliripotiwa kupoteza maisha katika pambano hilo hilo la mjini Tokyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img