15 C
New York

McTominay ndani tuzo za Ballon d’Or

Published:

MANCHESTER, England
UKIWA ni mwaka mmoja tu umepita tangu alipoondoka Manchester United, Scott McTominay ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuiwania tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.
Kiungo huyo raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 28, ambaye ni mara yake ya kwanza kuiwania tuzo hiyo, kwa sasa ni kipenzi cha mashabiki wa Napoli kutokana na kiwango chake bora ndani ya uwanja.
Msimu uliopita, ukiwa ni kwanza kwake klabuni hapo, aliipa Napoli taji la Ligi Kuu ya Italia (Serie A), akifunga mabao 13 na kutoa ‘asisti’ sita katika mechi 36 alizoshuka dimbani.
Baada ya kupoteza nafasi ya kuanza katika kikosi cha Man United, McTominay aliondoka na kujiunga na Napoli, uhamisho uliofanyika Agosti, mwaka jana.
Itakumbukwa, Man United walipokea kitita cha Pauni milioni 25 na kuingia sokoni kumsajili Manuel Ugarte aliyekuwa PSG.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img