DOHA, Qatar
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Qatar, Al Sadd, wamemsajili na kumpa mkataba wa miaka miwii mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Roberto Firmino.
Nyota huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 33, amejiunga na klabu hiyo akitokea Al Ahli Jeddah ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia.
Firmino alisajiliwa na Al Ahli wakati wa dirisha kubwa la kiangazi la mwaka 2023 akitokea Liverpool.
Akiwa Al Ahli, staa huyo alifunga mabao 21 na kutoa ‘asisti’ 17 katika mechi 65 alizocheza.
Pia, mchango wake huo wa mabao uliiwezesha timu hiyo kulibeba taji la Ligi ya Mabingwa barani Asia.
Katika mabao hayo, sita alifunga kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa, pia akitupia asisti mbili katika mechi ya fainali dhidi ya Kawasaki Frontale ya Japan.
Awali, kabla ya uamuzi wa kuelekea Qatar, Firmino alikuwa akihusishwa na mpango wa kurudi kwao, Brazil, au kujiunga na moja ya klabu za Uturuki.
Published:


